Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Sisi ni nani?

Wakala wa Serikali Mtandao ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kupitia sera na sheria mbali mbali kama vile malengo ya Zanzibar ya Dira 2020, Mpango wa Kondosha Umasikini Zanzibar I & II (MKUZA), sera ya utumishi wa Umma na Sheria  Na 2. ya utumishi wa umma ya mwaka 2011.

Kupitia sheria na.2  kifungu cha 97 ya utumishi wa umma  hizo imeipa wakala  jukumu la kushughulikia mambo yote yanayohusiana uendelezaji na usimamizi wa mifumo, TEHAMA, utayarishaji wa Sera na Miongozo ya TEHAMA na matumizi salama ya TEHAMA ndani ya utumishi wa umma. 

 Dira

Kuwa na serikali mtandao yenye ufanisi kwa ajili ya utawala bora.

Dhamira

 • Kutoa huduma za serikali kwa umma kwa ufanisi wa hali ya juu pamoja na Kusimamia utawala bora kwa kuzingatia misingi ya usalama na uaminifu.

 Malengo:

 •  Kuwa na kituo kimoja kinachosimamia maendeleo na matumizi ya TEHAMA ndani ya Utumishi wa Umma hali inayopelekea uthabiti katika udhibiti wa masuala ya TEHAMA.
 • Kuwepo kwa mamlaka yanayokidhi matakwa ya kisera na kisheria ya Serikali katika kustawisha Serikali mtandao.
 • Kuwa na nyenzo kisheria kwa ajili ya kusimamia miundombinu ya pamoja itakayowezesha upashanaji habari kwa urahisi, usalama na gharama nafuu.
 • Kuwa na muelekeo wa pamoja na mipango jumuishi ya maendeleo na matumizi ya TEHAMA ndani ya Utumishi wa Umma.
 • Kuongeza tija na ufanisi katika uendeshaji wa sekta ya umma kwa kuwepo na mawasiliano ya haraka, uhakika na salama kati ya vyombo mbalimbali vya Serikali.
 • Kupanua wigo wa upatikanaji taarifa katika kila ngazi ya Serikali, na mahitaji mbalimbali ya taarifa baina ya Serikali na wananchi, wazalishaji, wawekezaji na wadau wote ndani na nje ya nchi.
 • Kustawisha imani ya wananchi kwa serikali mtandao na Serikali yenyewe kwa kufanyika ukaguzi unaojitegemea unaohusisha fedha, utendaji kazi na mifumo ya TEHAMA.
 • Kuwepo kwa mipango maalum inayoratibu maendeleo ya watendaji ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA na maendeleo ya wataalamu wa TEHAMA ndani ya Utumishi wa Umma.
 • Kufanyika kwa tafiti zenye tija katika uimarishaji wa utoaji na upatikanaji huduma na utendaji serikalini kwa njia ya matumizi bora ya TEHAMA.
 • Kuongeza wigo wa vyanzo vya rasilimali zinazowezesha utekelezaji wa majukumu ya serikali mtandao.
 • Kupunguza gharama kwa kila ofisi ya Serikali inayohitaji huduma za TEHAMA, na kuwa na mfumo jumuishi wa mawasiliano unaowafikia walengwa wote.

Sheria ya Utumishi wa Umma iliyowezasha uwepo wa Wakala wa Serikali Mtanda

 • Sheria Na 2. ya mwaka 2011 ya Utumishi wa Umma
 • Mpango Mkakati wa Idara ya Serikali Mtandao
 • Zanzibar ICT Strategic Planning 
 • ICT Strategic Planning for Zanzibar.
 • Sera ya Taifa ya TEHAMA
 • NationaL ICT Policy
 • eGoz ICT Policy