Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Ujumbe wa Mkurugenzi

Ninayo furaha ya kukukaribisha katika tovuti ya wakala wa serikali mtandao, tunatuamaini utapata habari zenye kuaminika na zilizo kamili zitakazokupa muongozo kuhusu dira, muelekeo, malengo mikakati, shughuli kuu pamoja na maadili ya wakala.

Lengo kuu la tovuti hii ni kufikia miongoni mwa matarajio ya wakala ya kuendeleza na kurahisisha matumizi ya Tehama ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuboresha mfumo wa utoaji wa huduma katika wizara, idara na taasisi mbali mbali za serikali kwa ajili ya wananchi. Tutajitahidi kuendeleza malengo na ya ualinzilishi wa serikali mtandao kupitia sekta mbali mbali za serikali pamoja na kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na mawizara, taasisi, idara na sekta mbali mbali za umma na binafsi.

Tovuti hii inatarajia kuendelea kutoa taarifa mbali mbali kuhusiana na hatua madhubuti pamoja  mikakati imara inayochukuliwa na  Serikali kupitia Wakala wa Serikali Mtandao katika kutekeleza utekelezaji wa MKUZA II 2020 pamoja na kutimiza malengo ya wakala kama yalivyoelezwa katika mipango mkakati na sera ya Serikali Mtandao

Ni matumaini yangu kwamba tovuti hii itakuwa ni bora na yenye kutoa taarifa sahihi na kwa wakati. Nia yetu ni kuiboresha tovuti hii kila baada ya muda ili kurahisisha upatikana wa taarifa na huduma kwa wananchi wote wa Tanzania na wageni wa ndani wa nje  ya nchi.

Shukrani

Wakala wa Serikali Mtandao 
Zanzibar