Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Muundo wa Wakala

Kazi za kila siku za wakala zinasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao akisaidiwa na wakuu wa divisheni nne (4) kama vifuatavyo.

  1. Mtandao itakuwa na Divisheni za kiutendaji zifuatazo:
  2. Huduma za Kielektroniki na Mipango
  3. Usimamizi wa Miundombinu
  4. Utengenezaji wa Mifumo
  5. Msaada wa Kiufundi na Viwango

DIVISHENI YA HUDUMA ZA KIELEKTRONIKI NA MIPANGO (E-SERVICES AND PLANNING)

Divisheni hii itakuwa na kazi ya kusimamia, kuratibu, kuandaa miongozo, mipango, kufanya tafiti zinazokuhusiana na masuala TEHAMA. Aidha divisheni itakuwa na jukumu la kutayarisha mependekezo yanayo husiana na utekelezaji wa mifumo ya kielektroniki itakayohitajika kusimamiwa na kutengenezwa katika Utumishi wa Umma pamoja na Kusimamia miradi ya Serikali Mtandao.

DIVISHENI YA USIMAMIZI WA MIUNDOMBINU (INFRUSTRUCTURE MANAGEMENT)

Divisheni hii itakuwa na kazi ya kusimamia miundombinu mbali mbali itakayowezesha kupatikana matumizi mazuri na kuleta faida ya Serikali Mtandao.

DIVISHENI YA UTAYARISHAJI WA MIFUMO (SYSTEM DEVELOPMENT)

Divisheni hii itakuwa na kazi ya kutayarisha mifumo mbali mbali itakayopendekezwa na Wakala ama Taasisi nyengine kwa ajili ya kutekeleza ukamilishaji wa dhana ya Serikali mtandao

DIVISHENI YA HUDUMA ZA KIUFUNDI NA VIWANGO (BUSINESS SUPPORT AND CONTROL)

Divisheni ya hii itakuwa na kazi za kutoa huduma za kifundi za kieletroniki katika taasisi za umma, kusimamia miongozo, viwango na kuhakikisha kuwa taasisi zote zinafuata taratibu zilizowekwa. Kutoa elimu ya matumizi ya mifumo katika taasisi za umma. Kupokea malalamiko au maoni ya watumiaji wa mifumo, miundo na huduma na kuwasilisha kwa wahusika ndani ya Idara.

Aidha chini ya kila divisheni kuna vitengo vilicyoundwa ili kutekeleza majukumu ya Wakala.