Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Majukumu ya Wakala

>> Kuandaa na kusimamia sera, kanuni na miongozo ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma.

>> Kuoanisha na kuratibu shughuli za Serikali Mtandao kwenye taasisi za umma kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.

>> Kuendeleza mipango ya TEHAMA katika taasisi za umma kwa madhumuni ya kurahisisha upashanaji wa habari.

>> Kuwawezesha watendaji wa Serikali katika matumizi ya TEHAMA ili kufikia hatua bora za utoaji huduma.

>> Kuwezesha na kuratibu maendeleo na kukuza shughuli za utoaji huduma za Serikali kwa njia za kielektroniki na kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi.

>> Kutoa miongozo juu ya ununuzi wa vifaa vyote vya TEHAMA katika Utumishi wa Umma

>> Kuhakikisha usalama wa mifumo ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma.

>> Kutayarisha na kufanya kampeni ya kuinua uelewa wa wananchi juu ya huduma zinazotolewa kupitia Serikali Mtandao.

>> Kutoa ripoti juu ya maendeleo ya utekelezaji wa Serikali Mtandao na mafanikio yake kwa Serikali na jamii kwa ujumla