eGov Agency
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kwamba maonyesho ya Utalii yanayofanyika Zanzibar ni muhimu kwa Serikali na wananchi kwa kuwa yamelenga kuitangaza Zanzibar na sekta ya utalii ambayo ndio muhimili mkuu wa uchumi. Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya hoteli ya Verde, Mtoni Mjini Zanzibar katika ufunguzi wa maonyesho ya Utalii Zanzibar ya mwaka 2018 ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, wadau wa utalii na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali pamoja na wananchi. Katika maelezo hayo, Rais Dk. Shein alisema kuwa Utalii umekuwa ukichangia asilimia 27 kwa Pato la Taifa na asilimia 80 ya fedha za kigeni zinazokusanywa ambapo muda wanaokaa watalii nchini umeongezeka ambapo hivi sasa mtalii hutumia wastani wa…
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameridhia Maonyesho ya Utalii Zanzibar yaendelee kufanyika kila mwaka kwa lengo la kuendelea kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii. Dk. Shein alitoa kauli hiyo huko katika ukumbi wa Hoteli ya Verde, Mtoni, Mjini Zanzibar katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi walioshiriki vyema katika sekta ya utalii ikiwa ni hatua za kukamilisha Maonyesho ya Utalii Zanzibar ya mwaka 2018 yaliaoza tarehe 17 mwezi huu. Hafla hiyo iliyokwenda sambamba na chakula maalum cha usiku ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Mama Mwanamwema Shein, viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali pamoja na wadau wa utalii wa ndani na nje ya Zanzibar. Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alitamka kuwa ameridhia kuendelea kufanyika kwa Maoyesho ya Utalii Zanzibar kila mwaka kwani yana umuhimu mkubwa katika…
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) katika kuendeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na kueleza kuwa kuanzishwa kwa “Program ya Pamoja ya Zanzibar” (ZIP) itakuwa ni kichocheo cha mafanikio. Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mratibu mpya wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa eneo la Zanzibar Bi Dorothy Temu-Usiri. Dk. Shein alieleza kuwa kutokana na uzoefu mkubwa wa utendaji kazi wa Mratibu huyo ana matumaini makubwa kuwa program hiyo sio tu itasaidia kuimarisha maendeleo ya Zanzibar bali itasaidia sana katika kufikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini. Rais Dk. Shein alisema kwamba, malengo ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa Zanzibar yako wazi katika kila sekta na yanafahamika kwa wananchi wote wa Zanzibar jinsi yalivyolenga katika kuimarisha sekta za maendeleo. Alisema kuwa…

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz