eGov Agency

Utengezaji wa Tovuti za Serikali

Idara ya Serikali Mtandao, miongoni mwa huduma zake za kila siku, inatoa huduma ya utengenezaji website za kisasa zenye tabia ya kuendana na mazingira ya vifaa vya electroniki unavotumia. Idara kupitia uhakiki wake ulioufanya mwaka jana, wa huduma za kielectoniki zinazotolewa kwenye taasisi nyingi za serikali, imeona kuna uhaba mkubwa wa tovuti, taasisi nyingi za serikali hazina tovuti na chache ambazo zipo bado ni za mifumo ya zamani, na haziendani na techonojia ya kisasa ya utengenezaji wa website, ijulikanayo kama " Responsive WebSite". 

Hivyo, idara imeona ipo haja ya kueka huduma hii, kwa taasisi yeyote ya serikali ambayo inahitaji website ya kisasa, ambayo utaweza kuifungua kupitia desktop, laptop, tablet au simu yako ya mkononi na iweze kukuonesha uhalisia wake bila ya kuzingatia kifaa unachotumia, basi idara tayari inatoa huduma hii kupitia kitengo chake cha Usanifu wa Mfumo, katika uniti ya Web development.

Kwa mawasiliano zaidi ya huduma hii, unaombwa utuandikie kupitia anuani zetu za hapo chini.

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz