eGov Agency

Intaneti ya Serikali

 Idara ya Serikali Mtandao, inatoa huduma ya interneti kwa taasisi nyengine za serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Huduma hii inapatikana kwa taasisi za serikali ambazo zimeshaunganishwa kwenye mkonga wa mawasiliano. Taasisi yeyote ya serikali inayo haki ya kuitumia huduma hii mara tu baada ya kuwasiliana na idara yetu, na kukamilisha ununuzi wa vifaa vinavohitajika ambavyo vitatumika kupokea huduma hiyo. Idara ya Serikali Mtandao inaendelea kuimarisha huduma hii, ili iwe bora zaidi na kupatikana kwa kasi ya uhakika.

Idara ya serikali mtandao kwa kushirikiana na wizara ya mawasiliano, inaendelea na kuziunganisha taasisi za serikali, Unguja na Pemba ili ziweze kufaidika na huduma hii, kwa mpaka sasa ni zaidi ya taasisi 100 zimeshaunganishwa na zinatumia huduma hii kwa kazi za kila siku. Taasisi yeyote ambayo inahitaji kupata huduma hii, inashauriwa kuwasiliana na Idara ya Serikali Mtandao, kwa kutumia anuani zinaoonekana kwenye tovuti hii. Kwa hatua za awali, idara husika inaombwa wawe na mfumo wa ndani wa mawasilinao, yaani LAN ili iwe rahisi kwa hatua zozote zitazofuata ili waweze kupatiwa huduma hii.

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz