eGov Agency

Ujumbe wa Mkurugenzi

Mtendaji Mkuu wa Idara ya Serikali Mtandao 

Ninayo furaha ya kukukaribisha katika tovuti ya idara ya serikali mtandao, tunatuamaini utapata habari zenye kuaminika na zilizo kamili zitakazokupa muongozo kuhusu dira, muelekeo, malengo mikakati, shughuli kuu pamoja na maadili ya idara.

Lengo kuu la tovuti hii ni kufikia miongoni mwa matarajio ya idara ya kuendeleza na kurahisisha matumizi ya Tehama ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuboresha mfumo wa utoaji wa huduma katika wizara, idara na taasisi mbali mbali za serikali kwa ajili ya wananchi. Tutajitahidi kuendeleza malengo na ya ualinzilishi wa serikali mtandao kupitia sekta mbali mbali za serikali pamoja na kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na mawizara, taasisi, idara na sekta mbali mbali za umma na binafsi.

Tovuti hii inatarajia kuendelea kutoa taarifa mbali mbali kuhusiana na hatua madhubuti pamoja  mikakati imara inayochukuliwa na  Serikali kupitia idara ya Serikali Mtandao katika kutekeleza utekelezaji wa MKUZA II 2020 pamoja na kutimiza malengo ya idara kama yalivyoelezwa katika mipango mkakati na sera ya Serikali Mtandao

Ni matumaini yangu kwamba tovuti hii itakuwa ni bora na yenye kutoa taarifa sahihi na kwa wakati. Nia yetu ni kuiboresha tovuti hii kila baada ya muda ili kurahisisha upatikana wa taarifa na huduma kwa wananchi wote wa Tanzania na wageni wa ndani wa nje  ya nchi.

 

Shukrani

Mkurugenzi 
Idara ya Serikali Mtandao 
Zanzibar

 

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz

Anuani

Idara ya Serikali Mtandao
: Mazizini
 : +255 24 22 35689
: info@egoz.go.tz
: www.egoz.go.tz