Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Msaada wa Ushauri na Ufundi

Wakala wa Serikali Mtandao ikiwa ndio msimamizi mkuu wa masuala ya tekonolojia Habari na Mawasiliano katika Taasisi za Umma, inatoa ushauri katika  uanzishwaji wa mifumo yote ya ICT katika taasisi za Serikali, manunuzi ya vifaa vya TEHAMA na mambo yanayohusiana na TEHAMA .Wakala Serikali Mtandao, hutoa ufafanuzi wa vigezo mbali mbali vinavopaswa kuzingatiwa katika kuanzisha mifumo mipya au kuboresha iliopo pamoja na vigezo vya vifaa vya TEHAMA kulingana na mahitaji yanayotakiwa. Wakala hushirikiana na Tasisi husika hatua kwa hatua mpaka kukamilika kwa mfumo ulioanzishwa au kukamilka kwa manunuzi ya vifaa vinavyohitajika na kuhakikisha kuwa yanaendana na miongozo na viwango vilivyoekwa na wakala.