Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Barua pepe za Serikali

Wakala wa Serikali Mtandao, inatoa huduma ya barua pepe au email kwa watumishi wa taasisi za serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Email hizi zimetengenzwa maalum kwa ajili ya kusaidia mawasiliano ya kila siku ya kikazi kwa watumishi wa Umma. Mfumo wa barua pepe umeshatumiwa katika taasisi na baadhi ya watumishi kwa mda sasa, na umekua ukisaidia kwa ufanisi mkubwa katika utendaji wa kila siku, kwa mfano wa kutuma documents na file kutoka sehemu moja kwenda nyengine. Kutokana na uchache wa barua pepe zilizokuepo mwaanzo, wakala imechkua hatua kubwa katika kuhakikika kwamba kila mtumishi anapata barua pepe ili iweze kusaidia mawasiliano katika taasisi yake.

Wakala imejipangia hadi ifikapo mwakani, kila mtumishi awe na barua pepe yake, kwa hivyo maandalizi ya kutengeneza na kugawa barua pepe mpya yameanza, na kazi inaendelea vizuri. Kwa mfanyakazi yeyote wa serikali ambae tayari anahitaji barua pepe hizi kwa haraka zaidi, tunaomba usisite kuwasiliana nasi kupitia anuani zetu zilizopo ndani ya tovuti hii ili uweze kupatiwa barua pepe yako au za taasisi yako.